Home Uncategorized JEMBE JIPYA AZAM FC LAPANIA KUTUPIA MABAO ZAIDI YA 15

JEMBE JIPYA AZAM FC LAPANIA KUTUPIA MABAO ZAIDI YA 15


 MPIANZA Monzinzi ingizo jipya ndani ya Klabu ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina amesema kuwa hesabu zake ni kufunga mabao mengi ndani ya timu hiyo ili kuipa mafanikio makubwa.

Nyota huyo ambaye awali aliwekwa kwenye hesabu za Yanga kabla ya kuibukia ndani ya Azam FC amesaini dili la mwaka mmoja akitokea Academic Club Rangers ambayo ndiyo inammiliki ila alikuwa anacheza kwa mkopo ndani ya Klabu ya FC Lupopo.

Amekuja ndani ya Azam FC kuziba pengo la mshambuliaji Akono Akono Thiery ambaye amesepa ndani ya Azam FC na kuibukia nchini Malysia.

Nyota huyo amesema:”Nimekuja kufanya kazi ndani ya Azam FC na nina amini kwamba hilo litawezekana kwa kuwa timu ni bora na ina mwalimu mzuri pamoja na wachezaji wenye uwezo mkubwa.

“Imani yangu ni kwamba tutafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na malengo yangu ni kuona ninafunga mabao mengi hasa mzunguko wa pili.

“Ninahitaji kuona ninafunga mabao zaidi ya 15 kuanzia 20 hivi itakuwa furaha kwangu ila kikubwa ni timu kupata matokeo ndani ya uwanja,” amesema.


Azam FC ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza jumla ya mechi 17 kibindoni ina pointi 32.

SOMA NA HII  MASHINE MPYA YA SIMBA YAJIPA KAZI YA KUFANYA