Home Habari za michezo WALE WANAOBEZA KUREJEA KWA LUIS MIQUISSONE WATULIE KWANZA, VIGOGO SIMBA WAFUNGUKA

WALE WANAOBEZA KUREJEA KWA LUIS MIQUISSONE WATULIE KWANZA, VIGOGO SIMBA WAFUNGUKA

Habari za Simba

UONGOZI Simba, umeweka wazi kuwa, wale watu wanaobeza wao kumrejesha Luis Miquissone, watulie kwani watamshangilia huko mbeleni baada ya kushangazwa na uwezo atakaouonesha.

Winga huyo amerejea Simba baada ya kuvunja mkataba wake Al Ahly ambapo kabla ya kuondoa kikosini hapo, aliweka ufalme ndani ya Simba jambo ambalo kwa sasa watu wanatarajia kumuona akirejesha ufalme wake.

Akizungumza na Mwandishi , Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally, Alisema: “Wale ambao wanambeza Luis Miquissone kwa nini amechagua kurudi ndani ya Simba, ndio haohao ambao watakuja kumshangilia pale ambapo atakuja kufanya mabalaa yake.

“Kwetu sisi hatuna shaka na uwezo wa Luis Miquissone kwamba tuwe na hofu ya kumrudisha kwani tunatambua uwezo wake ni wa aina gani, Luis ni moja kati ya wachezaji wakubwa sana, na ndani ya Simba atawashangaza watu wengi.

“Kwa sasa niwaambie tu Wanasimba wote kuwa mnachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanakuja kwa wingi sana katika Tamasha la Simba Day kujionea ubora wa wachezaji wao na jinsi gani ambavyo tamasha linafanyika kwa ubora mkubwa sana,” alisema kiongozi huyo.

Kwa upande wa Luis ambaye msimu wa 2020/21 katika Ligi Kuu Bara alitoa asisti 9, amesema: “Nimekuja kwa ajili ya kufanya kazi na ninaamini kwa kushirikiana na wenzangu tutawapa furaha mashabiki wa Simba na kutimiza majukumu yetu.”

SOMA NA HII  HILI HAPA JESHI RASMI LA SIMBA DHIDI YA AFRICAN LYON, KOMBE LA SHIRIKISHO