Home Habari za michezo SIKU CHACHE BAADA YA KUSAJILIWA SIMBA…KAPAMA AIBUKA NA HILI KUHUSU MKUDE..ADAI AMEKUWA...

SIKU CHACHE BAADA YA KUSAJILIWA SIMBA…KAPAMA AIBUKA NA HILI KUHUSU MKUDE..ADAI AMEKUWA AKIMPA SHIDA SANA…


Kiraka mpya wa Simba, Nassoro Kapama amesema endapo kocha Zoran Maki atamchezesha kiungo namba sita na Jonas Mkude, basi kuna kitu kikubwa kitafanyika.

Kapama ametambulishwa na Simba juzi akiwa amesaini mkataba wa miaka miwili, amesema kuwa anamudu nafasi nyingi uwanjani lakini anafurahi zaidi akichezeshwa kiungo mkabaji.

Mchezaji huyo ambaye alikiri kuwa na ndoto ya kucheza pamoja na Mkude alisema amekuwa muumini wa kumfuatilia kiungo huyo hivyo baada ya kupata nafasi ya kucheza naye pamoja anatamani kupangwa mechi moja. “Moja ya viungo ambao tukikutana kwenye mechi wamekuwa wakinipa shida ni Mkude na ni mchezaji ambaye nimekuwa nikimfuatilia na kujifunza vitu kutoka kwake nimefurahi kucheza naye timu moja,” alisema.

“Tukipewa mechi moja pamoja yaani tukacheza pacha ya kiungo mkabaji kuna kitu kikubwa tutakifanya kwasababu kuna vitu ninavyo Mkude hana na kuna vitu anavyo mimi sina tukichanganya mechi hiyo wapinzani watalala na viatu.”

“Wanasimba watarajie mambo mazuri kutoka kwangu, nimekuja kufanya nilichonacho kwa kuchanganya na kile nitakachokikuta kwa wachezaji wenzangu, nahitaji ushirikiano wa kutosha.”

SOMA NA HII  HAYA HAPA USIYOYAJUA KUHUSU SHOMARI KAPOMBE...KILA GAME ANA DAKIKA ZAKE AISEE