Home Azam FC KOCHA AZAM FC AWATEMEA MBOVU WACHEZAJI…AMEZUNGUMZA HAYA

KOCHA AZAM FC AWATEMEA MBOVU WACHEZAJI…AMEZUNGUMZA HAYA

AZAM FC WAGOMEA MAKOCHA WABONGO...IBENGE KUMWAGA WINO

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Kally Ongala ameichifua kuwa, kwenye timu hiyo hakuna supastaa na mchezaji yeyeote anaweza kuanzia benchi na bado timu ikapata ushindi kama kawaida.

Kauli ya Ongala imejiri baada ya kuwaweka baadhi ya wachezaji wa timu hiyo benchi juzi usiku wakati Azam ikiizamisha tena Mtibwa Sugar kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa Azam Complex, akiwemo Prince Dube na Kipre Junior ambao ni tegemeo wa kikiosi hicho.

“Unapokuwa na wimbi la wachezaji wengi bora unaamua leo aanze huyu na kesho yule kwa sababu hawatofautiani sana na hilo ndilo ambalo sisi kama benchi la ufundi tulikuwa tunalihitaji kutokana na kushiriki mashindano mengi.”

Ongala aliongeza mwenendo wa timu kwa sasa ni mzuri ingawa bado wana kazi kubwa ya kufanya ili wasitetereke kwani malengo yao ni kumaliza nafasi tatu za juu licha ya washindani wao Singida Big Stars kutishia nafasi hiyo.

Katika mchezo huo uliopigwa kuanzia saa 3:30 usiku, Azam ilishinda mabao 2-1 yaliyofungwa na Isah Ndala na Idd Seleman ‘Nado’, huku bao la kufutia machozi la Mtibwa likifungwa na Onesmo Mayaya.

Ushindi huo kwa Azam ni wa pili mfululizo dhidi ya Mtibwa kwani kabla ya hapo iliwafunga mabao 2-0 na kuitoa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) katika hatua ya robo fainali iliyochezwa Aprili 3 na kwenda nusu fainali na sasa itavaana na Simba kwenye hatu

SOMA NA HII  HIZI HAPA REKODI ZA KUTISHA ZA WYDAD CA...SIMBA WAJIPANGE HASWAA!!