Home Simba SC SIMBA YATOSHANA NGUVU TENA MOROCCO, KIKOSI KUREJEA JUMA HILI TANZANI

SIMBA YATOSHANA NGUVU TENA MOROCCO, KIKOSI KUREJEA JUMA HILI TANZANI


KATIKA mchezo wa kirafiki ambao Simba wamecheza leo dhidi ya Olympique Club wametoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Huu unakuwa ni mchezo wa pili kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Didier Gomes ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.

Ule wa kwanza walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 dhidi ya FAR Rabat ya Morocco. 

Kikosi hicho kinatarajiwa kurejea mwishoni mwa juma hili ili kuendelea na maandalizi ya mwisho kuelekea katika msimu mpya.

Kwa ardhi ya Tanzania leo pia Simba walizindua App yao maalumu kwa ajili ya kuwapa taarifa mashabiki wake.

SOMA NA HII  SIMBA YAKIMBILIA CAF MECHI NA WYDAD...VAR ITATUMIKA...MANULA,KANOUTE OUT