Home Habari za michezo SIMBA NI NGUMU ILA INAFUNGIKA

SIMBA NI NGUMU ILA INAFUNGIKA

FT: TZ PRISONS 1-3 SIMBA SC

Kiungo mkabaji wa Singida Big Star, Morice Chukwu amekiri mechi itakayopigwa kesho wakiwa nyumbani dhidi ya Simba ni ngumu, lakini ametamba inafungika ikizingatiwa mchezo wenyewe unachezwa Uwanja wa Liti mjini Singida.

Timu hizo zitavaana huku kila moja ikitoka kupata ushindi kwenye mechi zilizopigwa ugenini juzi, Simba ikiifumua Tanzania Prisons kwa mabao 3-1, huku Singida ikiichapa Mtibwa Sugar kwa bao 1-0 lililowekwa wavuni na Mkenya Elvis Rupia.

Akizungumzia mchezo huo unaomkutanisha na Simba aliyowahi kuhusishwa kujiunga nayo, Chukwu alisema katika timu zote za ndani msimu huu tangu atue nchini Wekundu hao ndio wamekuwa bora kwao akikumbushia mechi ya Ngao ya Jamii iliyopigwa Agosti 8, Mkwakwani na kuisha kwa sare kabla ya kutolewa kwa penalti 4-2.

Alisema mechi ya kesho inaonekana kuwa mgumu, lakini wamepania kushinda. “Nimecheza mechi kadhaa hapa Tanzania, lakini Simba ndio imekuwa timu ngumu mpaka sasa. Wana timu yenye wachezaji wakubwa unatakiwa kila wakati uwe mchezoni,” alisema Chukwu aliyesajiliwa kutoka Rivers United ya Nigeria.

“Tunakwenda kucheza mechi ngumu nyingine zaidi na Simba lakini naamini tutafanya vizuri kwa kuwa hata sisi tumeanza kukaa sawa.”

Msimu uliopita kwenye ligi uwanjani hapo, Simba ililazimika kuchomoa bao la kupata sare ya 1-1.

SOMA NA HII  SIMBA HAWATAKI UTANI KABISA, WENGINE WATATU WATAMBULISHWA SIO POA