Home Uncategorized NIYONZIMA AWAVUTA WAKONGWE WAWILI KASEJA NA KADO

NIYONZIMA AWAVUTA WAKONGWE WAWILI KASEJA NA KADO


 HARUNA Niyonzima kiungo wa Yanga amelazimika kuwavuta kwenye mazoezi ya pamoja wakongwe wenzake, Juma Kaseja na Shabani Kado, ikiwa ni mkakati mahususi wa kujiandaa na tamko la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) la kurejea kwa Ligi Kuu Bara.
Kufuatia kuwepo na taarifa za TFF kuwa katika mipango ya ndani ya kuirejesha ligi hivi karibuni, baadhi ya wachezaji kutoka klabu mbalimbali kama Juma Kaseja anayekipiga KMC, Shabani Kado wa Mtibwa Sugar na Niyonzima wameamua kuongeza muda wa mazoezi yao ya kila siku.
Niyonzima amesema kuwa, awali baada ya ligi kusimamishwa alikuwa akifanya mazoezi mara moja kwa siku nyumbani kwake kama alivyokuwa amepangiwa na kocha wake, Luc Eyamel, lakini kwa sasa ameungana na Kaseja na Kado ambapo wanafanya mara mbili kwa siku.

“Awali nilikuwa nafanya kweli mazoezi mara moja tena nyumbani maana kuna nafasi ya kutosha ambayo ilikuwa inaniwezesha kwenda na program za kocha, ila siku zinavyoenda nimelazimika kuongeza muda wa mazoezi ambapo sasa hivi nafanya na Kaseja pamoja na Kado.
“Mazoezi yetu mara kadhaa tunafanyia katika ufukwe wa Escape One pale Mikocheni na tumekuwa tukijitahidi sana kufanya mazoezi ambayo yanaweza kutufanya tuendelee kuwa na utimamu sahihi wa mwili ili hata kama zile taarifa za ligi kurejea zikikamilika basi zitukute tuko fiti,” amesema Niyonzima.
SOMA NA HII  YANGA YAFICHUA SIRI YA USHINDI KWA ALLIANCE