Home Uncategorized NYOTA HAWA WA SIMBA WAMPASUA KICHWA MBELGIJI

NYOTA HAWA WA SIMBA WAMPASUA KICHWA MBELGIJI

PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ana kazi ngumu ya kufanya kwa sasa baada ya nyota wake kujiunga na timu ya Taifa.
Kocha huyo amedai kuwa wachezaji hao wataharibu mipango yake kwenye mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na muda ambao watakaokaa ndani ya kambi ya Stars.
Aussems amesema kuwa wachezaji hao watarudi siku chache kabla ya mechi yao hiyo ya kimataifa ambapo wamepangwa kucheza na UD do Songo ya Msumbiji kati ya Agosti 9 hadi 11.

“Wachezaji hao ambao wameenda Stars, kwa namna fulani wametibua mipango yangu kwa sababu watarudi siku mbili kabla ya sisi kucheza na UD Songo.

“Wakija ni lazima wapewe mafunzo maalum ili wawe sawa na wenzao, kitu ambacho unaona kinatibua mbinu zangu,” amesema Aussems.

Aussems ataiongoza Simba kwenye michuano ya kimataifa kwa mara ya pili mfululizo ambapo kwa msimu huu watacheza na mabingwa wa Msumbiji UD do Songo.

 Mechi ya kwanza watacheza nchini Msumbiji Agosti 9-11 na watarudiana Dar es Salaam Agosti 23-25 na baadhi ya nyota ambao wapo timu ya Taifa ni nahodha John Bocco na Ibrahim Ajib.
SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA AZAM FC UWANJA WA TAIFA, ROBO FAINALI FA