Home Uncategorized DAU LA KIUNGO ANAYEWINDWA NA YANGA ACHA KABISA, AKUBALI KUTUA

DAU LA KIUNGO ANAYEWINDWA NA YANGA ACHA KABISA, AKUBALI KUTUA


WINGA wa AS Vita ya DR Congo, Tuisila Kisinda, anahitaji Sh milioni 340 za Kitanzania, ili aavae jezi ya timu ya Yanga  kwa msimu ujao wa 2020/21.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zikimuhusisha winga huyo kumalizana na Yanga ambayo inapata jeuri ya usajili kupitia wadhamini wao Kampuni ya GSM.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga, kililiambia Spoti Xtra kuwa, winga huyo tayari alishafanya mazungumzo na klabu hiyo na wamekubaliana kila kitu, kilichobaki ni kutumiwa fedha zake Sh Mil 340 ambazo uongozi ulimuahidi.
“Uongozi wa Yanga unaohusika na usajili ulishafanya mazungumzo ya awali na Tuisila na mazungumzo yameshakamilika, kilichobaki ni masuala ya fedha ambapo makubaliano ni mchezaji kupatiwa Sh milioni 340 ambazo ni ada ya usajili.
“Bado fedha hazijatumwa, wanachotaka kufanya Yanga ni kusubiri mipaka ya DR Congo ifunguliwe ili wakimtumia tu basi aweze kuungana na wenzake,” kilisema chanzo.
Alipotafutwa Kisinda, alisema: “Tayari nimeshafanya mazungumzo na Yanga na yamekwenda vizuri, kwa sasa nasubiri kutumiwa fedha za usajili ambazo tulikubaliana, fedha hizo ni siri yangu. Nikitumiwa tu nakuja Yanga.”

Kisinda ambaye pia anaitumikia timu ya taifa ya DR Congo, anatokea nchi moja na kiungo na nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi.
SOMA NA HII  AZAM FC YAFUNGASHIWA VIRAGO NA YANGA KOMBE LA MAPINDUZI