Home Habari za michezo BAADA YA KUONYESHA KIWANGO CHA ‘DUNIA’…KOCHA MSAUZI AIBUKA NA HILI KWA SALIM...

BAADA YA KUONYESHA KIWANGO CHA ‘DUNIA’…KOCHA MSAUZI AIBUKA NA HILI KWA SALIM ALLY…

KIPA CHIPUKIZI SIMBA AMWAGA SIRI NZITO...AMTAJA AISHI MANULA...ISHU IKO HIVI A-Z

Aliyekuwa Kocha wa Walinda Lango wa Simba SC Tyron Damons amekiri kumtumia ujumbe wa Pongezi Mlinda Lango chaguo latatu Ally Salim, kufuatia kuonesha kiwango kizuri katika michezo aliyobahatika kucheza msimu huu.

Mlinda Lango huyo amekuwa na bahati ya kucheza michezo mitatu mfululizo pasina kuruhusu bao, akicheza michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya (Ihefu FC, Young Africans) na mmoja wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wydad AC ya Morocco.

Kocha Damos ambaye aliondoka Simba SC mwanzoni mwishoni mwa msimu uliopita, alikua na msaada mkubwa kwa Ally Salim licha ya Mlinda Lango huyo kukosa nafasi ya kukaa langoni kwa wakati huo.

Kocha huyo raia wa Afrika Kusini amesema: “Nimemtumia ujumbe na amesema asante sana kwa kila jambo, nikamwambia wakati mwingine sio mimi ni watu wanaokuzunguka ukiwa tayari kujifunza na kujiboresha kazi itakuwa rahisi na hii inaitwa hatua wala sishangai”

“Mimi sitaki kuchukua sifa kwa sababu amefanya vizuri , unajua watu wengi wanaweza kunipigia simu na kunisifia, ndio kila mmoja anaweza kuchukua sifa lakini naona tumpe sifa kijana.”

Ally Salim alipata nafasi ya kukaa langoni baada ya kuumia kwa Mlinda Lango chaguo la kwanza Aishi Manula ambaye huenda akakosa sehemu ya msimu huu iliyosalia, kufuatia majeraha ya Bega yanayomkabili kwa sasa.

Licha ya uwepo wa chaguo la pili klabuni hapo Beno Kakolanya, Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Olivieira ‘Robertinho’ alimumini Salim na kumpa nafasi ya kukaa langoni katika mchezo dhidi ya Ihefu FC, ambao ulimalizika kwa Mnyama kupata ushindi wa 2-0.

Kisha akampa nafasi kwenye mchezo dhidi ya Young Africans iliyokubali kufumuliwa 2-0 na juzi Jumamosi (April 22) aliitetea Simba SC kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wydad AC ya Morocco.

SOMA NA HII  WEWEEH..AJIBU BADO YUPO SANA MSIMBAZI..AONGOZA NYOTA HAWA WAPYA KWENDA MOROCCO