Home Azam FC WAKATI SIMBA NA YANGA ZIKIWA KILELENI CAF….AZAM FC WAMEJIPIGAPIGA KIFUA KISHA WAKASEMA...

WAKATI SIMBA NA YANGA ZIKIWA KILELENI CAF….AZAM FC WAMEJIPIGAPIGA KIFUA KISHA WAKASEMA HAYA…

Azam FC

NYOTA wa Azam FC, Ayub Lyanga amesema mabao mawili aliyofunga kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting yameongeza chachu ya ushindani kwenye kikosi chao ambacho amekiri kuwa kinahitaji nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Ushindi walioupata Azam FC umewafanya wapande nafasi moja kutoka nne hadi tatu baada ya kukusanya pointi 53, wakiwashusha Singida Big Stars ambao wapo nyuma kwa mchezo mmoja wakiwa na 51 na Ruvu Shooting wameshuka hadi nafasi ya mwisho.

Lyanga alisema ni matokeo mazuri kwao na anafurahi kuwa miongoni mwa wachezaji walioipa matokeo ya ushindi timu yake ambayo ameweka wazi kuwa pamoja na kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi kimataifa bado wanaitaka nafasi ya tatu.

β€œUshindi tulioupata ugenini dhidi ya Ruvu Shooting unaturudisha imara nyumbani tukiwasubiri Namungo tutaingia mchezoni tukiwa kwenye hali nzuri ya ushindani.

β€œNimefunga mabao mawili siyo kwa juhudi zangu ni namna timu ilivyocheza kwa kushirikiana na kuelewana tutaendelea tulipoishia ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kupata matokeo nyumbani dhidi ya Namungo tukijiandaa na Simba hatua ya nusu fainali FA.”

Akizungumzia mchezo kwa ujumla alisema ulikuwa ni bora na wa ushindani kutokana na kukutana na timu ambayo inapambana isishuke daraja lakini ubora wakikosi chao umeamua matokeo mazuri.

Lyanga alisema duru la pili ni gumu kutokana na kila timu kupambana kuhakikisha inakusanya pointi zitakazowafanya wabaki msimu ujao hivyo wao kama wachezaji wanatambua hilo na kutumia jitihada binafsi ili kuipambania timu ipate pointi tatu muhimu.

SOMA NA HII  KISA KOSA KOSA ZA KWENYE MECHI YA SIMBA....NABI AWAPASUKIA UKWELI MASTAA YANGA SC...