Home Habari za michezo HIKI HAPA NDIO KILICHOWAPONZA YANGA DHIDI YA WAARABU

HIKI HAPA NDIO KILICHOWAPONZA YANGA DHIDI YA WAARABU

Kwenye hii michuano mikubwa unahitaji wachezaji wako wote wawe na siku nzuri kazini ili uweze kufanya vizuri.

Yanga jana wamem-miss Djigui Diarra golini hivyo build-up haikiwa sawa kwani Metacha siyo A ball playing goalkeeper.

Pia, kutokuwepo kwa Diarra kumewanufaisha Belouizdad kwenye Counter attack kwani Metacha siyo Sweeper keeper hivyo hana sifa ya kutoka golini mara kwa mara ili kuingilia Counter attack za wapinzani.

Pili.

Mudathir hakuwa sawa katikati ya uwanja muda mwingi alipoteza mipira iliyopelekea kupigwa Counter attack.

Tatu.

Ibrahim Bacca amecheza vibaya kipindi cha kwanza, goli la kwanza alitakiwa kuosha mpira hakufanikiwa Yanga wakafungwa bao la kwanza, goli la pili ilikuwa ni Counter attack 2v2 Job alikuwa sawa na mchezaji mwenye mpira hivyo Bacca alitakiwa kum-Mark Mfungaji Meziane, lakini aliachana nae na kupelekea bao hilo.

Nne:

Aziz na Maxi hawakuwa kwenye ubora wao hivyo Yanga wameathirika pakubwa. Mwisho kabisa Yanga wanahitaji namba 9 wa kuamua mechi kubwa kama hizi. All in All Yanga ni timu nzuri na bado wana nafasi kubwa ya kusonga mbele.

SOMA NA HII  NAMNA SIMBA WATAKAVYONUFAIKA NA PESA SAMATTA ASTON VILLA, RAGE AFUNGUKA