Home news MWANZILISHI WA SIMBA DAY ATIA HURUMA..ANAISHI KWA MATESO…AMTAJA MO DEWJI..SIMBA WATOA TAMKO…

MWANZILISHI WA SIMBA DAY ATIA HURUMA..ANAISHI KWA MATESO…AMTAJA MO DEWJI..SIMBA WATOA TAMKO…


INASIKITISHA, lakini ndivyo ilivyo hali ya Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Hassan Dalali ‘Field Marshall’ inatia huruma, kiasi huwezi kuamini kama huyu ni mmoja wa viongozi wa Msimbazi aliyefanya makubwa yanayoipaisha kwa sasa klabu hiyo.

Ndio, Dalali aliyeiongoza Simba kuanzia 2007-2010 na kuifanyia makubwa ikiwamo kuiachia Simba uwanja ambao umejengwa na sasa ukifahamika Mo Simba Arena, maisha yake halisi hayaendani na thamani ya jina alilonalo kwenye jamii.

Dalali amekimbizwa kwake kutokana na mafuriko yaliyoikumba nyumba yake iliyopo Magomeni Makanya, Dar es Salaam ambaKo kwa sasa amejihifadhi kwa mtoto wake wa kike aitwaye Ummi anayeishi eneo la Mbagala Maji Matitu.

Gazeti la Mwanaspoti lilikwenda kujihakikishia mazingira halisi ya nyumba yake hiyo, ilikuta imejaa maji na upande mmoja mabati yaliezuliwa na upepo.

“Kwa sasa sipo Magomeni, nilikimbizwa na mafuriko ndio maana mmenikuta hapa kwa mtoto wangu wa kike, wakati mwingine nakwenda kukaa kijijini Tanga,” alisema Dalali kwa sauti ya huzuni.

Alipoulizwa utumishi wake Simba umemnufaisha vipi na maisha yake ya kawaida naye alijibu; “Raha yangu ni kuiona timu inafanya makubwa, sikutanguliza maslahi yangu binafsi, ndio maana ukiwauliza niliofanya nao kazi watakueleza.

“Ukienda Simba ama Yanga kwa ajili ya kujinufaisha, basi huwezi ukafanya lolote la kuzipeleka timu hizo mbali, nashukuru Mohamed Dewji amekuwa akijitoa na hatua zinaonekana,” alisema.

Alienda mbali kwamba kitu anachokitamani kukiona akiwa hai ni uwanja wa timu hiyo kukamilika na kuwa wa kisasa, huku akitoa ushauri wake kwamba viongozi waanzishe mchakato wakumhusisha kila Mwanasimba kuchangia.

“Namaanisha waanzishe akaunti ili wapatikane watu wa kuzunguka na watu wa benki kila mkoa, kuwaambia wanachama mwenye Sh1000 awe anaingiza moja kwa moja kwenye akaunti, hilo litafanya uwanja ukamilike kwa uharaka,” alisema.

Gazeti la Mwanaspoti ilimtafuta Mwenyekiti wa Simba wa sasa, Murtaza Mangungu kuhusiana na maisha halisi ya Dalali, alishituka na kutaka kujua undani zaidi.

“Dalali ni mtu muhimu na mtu wetu, kama atakuwa na changamoto yoyote awasiliane nasi moja kwa moja, hatuwezi kumtupa kwa namna yoyote ile,” alisema Mangungu.

SOMA NA HII  WAKATI WAKIHAHA NA KOCHA....ANTONIO CONTE ATUMA UJUMBE HUU KWA AZAM FC YA BONGO...

Kabla ya kwenda kujionea uhalisia wa nyumba yake kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ aligusia jambo la Dalali kujengewa nyumba kwakuwa wazo la Simba Day ndiye aliyeliasisi.

“Mzee Dalali anastahili kufanyiwa makubwa, kwanza ndiye aliyeanzisha Simba Day hadi limeigwa na timu nyingine, amefanya mengi hivyo anastahili hata kujengewa nyumba,” alisema.