Home Habari za michezo SIMBA YAAMBULIIA MIL 188 TU…KIMENUKA MASHABIKI WACHARUKA HASWAA!!

SIMBA YAAMBULIIA MIL 188 TU…KIMENUKA MASHABIKI WACHARUKA HASWAA!!

SIMBA YAAMBULIIA MIL 188 TU...KIMENUKA MASHABIKI WACHARUKA HASWAA!!

MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya watani wa jadi Simba na Yanga uliopigwa Aprili 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam umeingiza kiasi cha Sh410 milioni.

Katika mchezo huo ambao Simba ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa na Henock Inonga na Kibu Denis, jumla ya mashabiki 53, 569 waliingia ambapo VIP A iliingiza watazamaji 340 kwa kiingilio cha Sh30, 000.

Watazamaji hao waliingiza jumla ya Sh 10, 200, 000 huku VIP B ikiingiza watazamaji 4160 kwa kiingilio cha 20, 000 hivyo kupatikana jumla ya kiasi cha fedha cha Sh 83 milioni.

VIP C iliingiza watazamaji 2004 kwa kiingilio cha Sh 15, 000 na kupatikana Sh 30, 060, 000 wakati jukwaa la rangi ya machungwa liliingiza watazamaji 10, 372 kwa kiingilio cha Sh 10, 000.

Watazamaji hao walichangia kupatikana kwa jumla ya Sh 103, 720, 000 huku jukwaa la mzunguko likiingiza watazamaji 36, 693 kwa kiingilio cha Sh 5000 na kupatikana Sh183 milioni.

Mgawanyo wa fedha hizo ni kwamba wenyeji wa mchezo huo Simba imechukua Sh188 milioni huku Baraza la Michezo Tanzania (BMT) likichukua kiasi cha Sh10 milioni.

Kodi ya Serikalini ni Sh62 milioni, gharama za tiketi ni Sh22 milioni, uwanja ni Sh47 milioni huku gharama za mchezo zikiwa ni Sh22 milioni.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limepata Sh12 milioni, Bodi ya Ligi (TPLB) Sh25 milioni huku Chama cha Soka Mkoa (FA) kikivuna Sh18 milioni.

Mdau na shabiki wa soka mkoani Iringa, Kefa Walles amesema kilichopatikana na kugawiwa kwa timu mwenyeji haviendani akieleza kuwa mgawanyo kwa baadhi ya maeneo haikustahili.

“Kama BMT ambao ni chombo cha serikali kusimamia michezo kina bajeti yake huu mgao hawakustahili, lakini hata FA kiwango hicho ni kikubwa sana, hizi timu zinatumia gharama kubwa mno kuanzia usajili hadi maandalizi ya mechi,” amesema Walles.

“Nadhani klabu zinapaswa kijitambua na kuangalia hasa maamuzi wanayofanya kwenye kupitisha kanuni, inatia shaka sana kama huwa wanasoma na kuelewa” amesema Edward Jackson mdau wa soka Mafinga.

SOMA NA HII  HAWA HAPA MASTAA 10 WALIOKIWASHA KISAWASAWA NA MAN UNITED...