Home Habari za michezo MANARA AIBUKA NA HAYA MAPYA…AWACHANA SIMBA MAKAVU LIVE…ALIVALIA NJUGA JAMBO HILI

MANARA AIBUKA NA HAYA MAPYA…AWACHANA SIMBA MAKAVU LIVE…ALIVALIA NJUGA JAMBO HILI

MANARA AIBUKA NA HAYA MAPYA...AWACHANA SIMBA MAKAVU LIVE...ALIVALIA NJUGA JAMBO HILI

Suala la kuondoka kwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba SC Abdelhak Benchikha na wasaidizi wake Farid Zemit na Kamal Bougnan, limemuibuka aliyewahi kuwa Afisa Habari wa Klabu hiyo ya Msimbazi Haji Sunday Ramadhan Manara.

Benchikha na wasaidizi wake wameondoka Simba SC, baada ya Uongozi wa klabu hiyo kuthibitisha kwa taarifa rasmi iliyochapishwa katika vyanzo vya taarifa vya klabu hiyo jana Jumapili (Aprili 28).

Manara amelivalia njuga suala hilo akisema kuna haja kwa viongozi wa Simba SC kubadilika na kuiga mfumo wanaotumia wenzao wa Young Africans ambao wamekuwa na mafanikio na furaha kwa mwaka wa tatu sasa.

Manara amesema Klabu ya Simba imekuwa ikiendeleshwa kwa mifumo ya kizamani na kusababisha kinachoendelea sasa ndani ya klabu hiyo, na kupelekea maumivu kwa Mashabiki na Wanachama wao ambao wamekuwa wakilalama kila kukicha kutokana na kinachoonekana nje na ndani ya uwanja.

SOMA NA HII  MENEJA WA KIBU DENIS AFANYA MAZUNGUMZO NA YANGA...AMEFUNGUKA HAYA A-Z