Home Habari za michezo BAADA YA MAYELE KUSHINDWA KUTWA KIATU CHA UFUNGAJI BORA..NABI AIBUKA NA HILI...

BAADA YA MAYELE KUSHINDWA KUTWA KIATU CHA UFUNGAJI BORA..NABI AIBUKA NA HILI KWA MPOLE..


Kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amempongeza mshambuliaji wa Geita Gold FC, George Mpole baada ya kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu 2021/22.

Mpole ametwaa kiatu cha ufungaji bora baada ya kufunga mabao 17 huku akimzidi mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele kwa bao moja ambapo alimaliza na mabao 16.

Nabi amesema wanampongeza Mpole kwa kuibuka kinara wa ufungaji huku akiongeza kuwa Mayele kwa sasa amevunjika moyo kwa kuwa baadhi ya mabao yake mawili yalikataliwa lakini pia muda mrefu ndio alikuwa anaongoza.

Aliweka wazi kuwa anaamini mchezaji huyo ametimiza malengo ya timu kwa maana ya kuipa ubingwa wa ligi na kesho anaenda kuipa tena ubingwa mwingine wa FA dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

SOMA NA HII  BAADA YA KELELE ZA MASHABIKI YANGA KUWA NYINGI...DJUMA AFUNGUKA HAYA..UONGOZI WATOA TAMKO