Home Uncategorized MAKOSA YA MSIMU ULIOPITA YAIPA SOMO SINGIDA UNITED

MAKOSA YA MSIMU ULIOPITA YAIPA SOMO SINGIDA UNITED

UONGOZI wa Singida United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Fred Minziro umesema kuwa makosa yaliyojitokeza msimu uliopita hayatatokea tena msimu mpya wa 2019/20.

Akizungumza na Salehe Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa wametambua namna walivyokwama kuleta ushindani msimu uliopita hali iliyofanya wajipange sawa kwa msimu ujao.

“Kwa nsimu uliopita haukuwa bora kwetu kutokana na namna tulivyoyumba na yote ilitokana na kukosekana kwa mdhamini ila kwa kuwa tumeshajua tulipokwama hesabu zetu ni kuyafuta makosa na kuanza upya,” amesema.

Msimu wa 2018/19 Singida United ilimaliza ikiwa nafasi ya 13 baada ya kujikusanyia pointi 46 kwenye michezo 38 waliyocheza.

SOMA NA HII  POGBA: NILIFANYA KOSA LA KIJINGA NDANI YA UWANJA