Home Uncategorized ALLIANCE FC WAMCHUNIA MALALE HAMSINI

ALLIANCE FC WAMCHUNIA MALALE HAMSINI

KOCHA wa Alliance FC, Malale Hamsini amesema kuwa tayari amemaliza mkataba wake ndani ya kikosi hicho hivyo kwa sasa yupo huru kujiunga na kikosi kingine kwa kuwa bado hajaitwa mezani.

Akizungumza na Salehe Jembe, Hamsini amesema kuwa kwa sasa hayupo na timu ya Alliance baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia timu hiyo.

“Nimemaliza mkataba wangu na Alliance hivyo bado sijaongeza mkataba mwingine kwa sasa, sijazungumza na uongozi wa Alliance kuhusu kuongeza mkataba wangu hivyo bado nipo huru,” amesema.

Malale ameiongoza Alliance kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 11 baada ya kucheza jumla ya mechi 38 ikiwa na pointi 47.

SOMA NA HII  MCHUNGAJI MASHIMO, MANARA HAPATOSHI!