Home Simba SC SIMBA:YANGA WANAMNGA’NGA’NIA MORRISON

SIMBA:YANGA WANAMNGA’NGA’NIA MORRISON

 BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa  Simba amesema kuwa Yanga wanamnga’nga’nia mchezaji wao wa zamani Bernard Morrison.

Nyota huyo ambaye alisaini dili la miaka miwili ndani ya Simba akitokea Klabu ya Yanga amekuwa kwenye mvutano na mabosi wake wa zamani hao kuhusu suala la mkataba wake.

Yanga wao wanaeleza kuwa nyota huyo ana mkataba wa miaka miwili ndani ya Yanga huku mchezaji mwenyewe akisema kuwa alisaini dili la miezi sita.

Sakata lake lilisikilizwa makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kwa muda wa siku tatu na mwisho wa siku waliamua kwamba mchezaji huyo ni huru kutokana na makosa ambayo yalikuwa kwenye mkataba wake.
 
Kutokana na matokeo hayo Yanga ilikata rufaa kwenye mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo,(CAS) ili kuweza kupata haki ya mchezaji wao.

Barbara amesema:”Kesi ya Morrison na Yanga bado ipo na kuna baadhi ya wanasheria wanatusaidia kwenye hiyo kesi.

“Naona Yanga bado wanahangaika. Ni kama upo kwenye mahusiano mnaachana halafu bado unamlazimisha mpenzi wako wa zamani arudi.

“Mmeachana, hakutaki, ameshaendelea na maisha mengine, bado unamng’ang’ania wa nini? Halafu mwenzio anamaisha yake hakusubiri. Achananae.”

Chanzo:Clouds

SOMA NA HII  BREAKING:SIMBA YAMTANGAZA MCONGO MPYA, YEYE NI BEKI