Home Habari za michezo HUYU NDIYE MO DEWJI BANAA….TAZAMA MPUNGA ANAOLIPA KWA SIMBA KUKAA DUBAI TU…

HUYU NDIYE MO DEWJI BANAA….TAZAMA MPUNGA ANAOLIPA KWA SIMBA KUKAA DUBAI TU…

Habari za Simba

Kibongobongo hapo ulipo unaeza kupiga chai ya kawaida kwa Shilingi laki moja na elfu 15?

Ndiyo kitakachokukuta ukithubutu kugusa tu chai kwenye hoteli waliyofikia Simba Dubai. Siyo ya kitoto. Kuna Mbongo ametikisa kichwa baada ya kunywa chai ya Sh 115,000.

Simba wameamua kutulia kwenye hoteli hiyo ya Arabian Park kwani ina kila kitu anachotaka Kocha wao mpya wa kikosi hicho, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ anayeiandaa Simba kushindana kimataifa.

Msafara wa Simba wenye watu 38, umeweka kambi kwenye hoteli ya kisasa ya Arabian Park ambako watakuwa kwa siku saba kwa mualiko wa rais wa heshima wa timu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo’

Hoteli hiyo imekuwa ikitumiwa na klabu mbalimbali kubwa duniani pindi zikiweka kambi Dubai, ina kila kitu, ikiwemo gym, viwanja vya mazoezi, Super Market yenye kila kitu muhimu ili kurahisisha maandalizi yao.

Ikiwa hapo, Simba inalipa dola 100 kwa usiku mmoja kwenye kila chumba ambacho nyota wake na viongozi wanalala, hapa ni Sh. 233, 500 kwa chumba kimoja ambapo jumla ni zaidi ya 60 milioni kwa siku saba ambazo watakaa hapo kwa ajili ya vyumba tu bila chakula na vinywaji ambavyo pia vinaelezwa kuwa ni ghali zaidi.

Jumla ya fedha hizo, unaweza kuona vile ambavyo tajiri huyo anamwaga mkwanja kutokana na msafara wa timu hiyo ambayo itakuwa nchini humo kwa siku saba, achana na matumizi mengine.

Mbali na fedha hizo, mazingira ya viwanja zaidi ya vitatu ambavyo vipo hapo, gym kubwa pamoja na ulinzi wa hali ya juu ambao upo kwenye eneo hilo unawafanya wawe kwenye utulivu wa hali ya juu na kuishi kishua zaidi.

Akizungumzia kambi hiyo wakati wakiondoka nchini, Robertinho alisema;

“Ni uamuzi mzuri kwa uongozi kunipa muda wa kufanya mazoezi na kikosi kwa utulivu ili kuniwezesha kuwajua wachezaji nakuwapa mbinu zangu.”

Mara baada ya kurejea nchini kabla ya mikiki ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba itakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi Mbeya City utakaopigwa Januari 17, katika Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  AHMED ALLY AMJIBU KIBABE ALLY KAMWE