Home Habari za michezo AHMED ALLY AMJIBU KIBABE ALLY KAMWE

AHMED ALLY AMJIBU KIBABE ALLY KAMWE

Habari za Simba leo

Kutoka kwa semaji la CAF, Ahmed Ally….

Kwenye sanaa ya Mawasiliano hakuna katika nyie anaweza kunifikia hata robo ndo maana nyie mkaajiriwa 10 kwenye idara moja mie niko peke yangu na bado mabosi wenu wakanunua machawa wengi kwa ajili ya kuwasaidia nyie kazi.

Kusema wachezaji wetu wanatakiwa kuboresha viwango vyao ni kuwachonganisha na mashabiki? Kwani mashabiki hawakuona kama tumecheza chini ya kiwango?

Mimi ndo Msemaji wa Simba natakiwa kusema mazuri na madhaifu yetu ambayo yanaonekana hadharani.Nimeeleza madhaifu yetu na kuwaahidi wana Simba kuwa tunakwenda kufanya maboresho kipindi hiki ligi imesimama.

Yaani nimeelezea tatizo na suluhu yake.Wana Simba wameridhika na ukweli huo na sasa wanasubiri utekelezaji wa maboreshoSisi kuelezana ukweli nyie mnaumia nini, Mnataka tusiambiane ukweli tucheze chini ya kiwango kwa maslahi ya nani??

Kwenye kusifia nitasifia sana, tena kwenye eneo hilo hakuna anaeniweza kwenye dunia hii lakini ikiwa tofauti natakiwa niseme vilevile.Wapo wanaosema kama kiongozi natakiwa nikazungumze ndani sio public, Wapo sahihi ninayokwenda kuzungumza kwenye vikao vya ndani ni yale mazito na makubwa lakin kukumbushana kuboresha kiwango ni jepesi mno linafanywa hadharaniNyie bado wachanga sana kunielekeza Gwiji.

SOMA NA HII  BENCHIKHA AJA NAKULI HII SIMBA