Home Habari za michezo SIMBA HAWATAKI UTANI AISEEE…WAMALIZANA NA STARIKA HATARI LA MAGOLI KUTOKA UGANDA USIKU...

SIMBA HAWATAKI UTANI AISEEE…WAMALIZANA NA STARIKA HATARI LA MAGOLI KUTOKA UGANDA USIKU USIKU…


Mabosi wa Simba hawataki utani. Baada ya kuwasapraizi mashabiki kwa kufanya ishu ya kocha mkuu mpya kimyakimya kabla ya kumtangaza Zoran Manojlovic, nguvu zimehamia kwa wachezaji na juzi wameshusha straika mpya na fasta kumsainisha usiku mwingi.

Kama ulidhani mabosi wa Simba wamelala kwenye ishu za usajili umekosea, wamemalizana na kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya Uganda, Ceasar Manzoki.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kinaeleza mazungumzo ya Manzoki na mabosi hao yameenda vizuri na juzi usiku alisaini mkataba na kuondoka usiku huohuo Jijini.Alitua nchini kimya kimya na kufichwa kwenye hoteli moja iliyopo katikati ya Dar es Salaam.

Chanzo hicho cha kuaminika kinaeleza Manzoki alikutana na mabosi hao wa Simba na kukubaliana kila kitu na ataanza kazi ya kuitumikia wikichache zijazo kama Moses Phiri.

Manzoki baada ya kumaliza jambo hilo alichukua ndege na kurudi Uganda kimya kimya bila ya kutaka mtu yeyote afahamu jambo hilo hadi hapo Simba itakapokuja kumtambulisha.

Inaelezwa suala hilo Manzoki amelifanya kimya kimya hadi kutua nchini kutokana na mabosi zake wa Vipers kutaka kumzibia kwa madai bado ana mkataba mwingine mbele wa miaka miwili, huku mchezaji akiruka kwa maelezo alisaini wa miaka miwili tu na timu hiyo ambayo msimu huu umemalizika na huo mwingine wala hautambui.

Manzoki ameamua kuwa mpole huku akimalizana na Simba kimya kimya ili aweze kupata barua (Release Letter) ambayo itawapa ruhusa mabosi zake wapya kumtangaza kama mchezaji wao mpya iliyomnasa kutokea Vipers ya Uganda.

Manzoki alisema yupo Uganda na suala lolote ambalo linahusu usajili kwa wakati huu analisimamia wakala wake.

“Nimeaga kule Uganda kupitia mitandao yangu ya kijamii kutokana na kazi nzuri niliyofanya msimu uliopita ila kuhusu mambo mengine pamoja na kuwepo Tanzania hilo si wakati wake kwa sasa,” alisema Manzoki ambaye hata wachezaji wa Ligi Kuu ya Uganda walimpigia kura ya kumpa uchezaji bora wa msimu kutokana na mbilinge zake.

SOMA NA HII  KIPIGO KUTOKA JANWENG CHAIBUA KIZAAZAA MSIMBAZI...MO DEWJI ATOA MSIMAMO...MAGORI ATAJWA

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez aliliambia Mwanaspoti wakati huu yupo bize kuhakikisha anapambana timu yake kufanya usajili mzuri kwa ajili ya msimu ujao.

“Tunaendelea kufanya mambo yetu kimya kimya, aamini tutasajili wachezaji wazuri ili kuongeza makali ya timu yetu msimu ujao, wqpenzi na mashabiki wa Simba watulie mambo mazuri yanakuja,” alisema Barbara ambaye anafanya mambo mengi ya kuirejesha klabu hiyo kwenye reli .

Msimu uliopita Manzoki akiwa na Vipers ya Uganda alimaliza msimu akiwa mfungaji bora akiweka kambani mabao 18, huku ikielezwa anakuja kuchukua nafasi ya Meddie Kagere atakayeachwa sikuchache zijazo.

Tayari Mwanaspoti lilikupa taarifa kutoka kwenye vyanzo vya uhakika ndani ya Simba imemalizana na Victor Akpan kutokea Coastal Union, Nassoro Kapama wa Kagera Sugar na Moses Phiri kutokea Zanaco ya Zambia. Endelea kutufuatilia.