Home Habari za michezo KISA ISHU YA SAIDO NA AMBUNDO KUSIMAMISHWA…MAYELE, SHABANI DJUMA WAJILIPUA YANGA…’WAMFESI’ NABI...

KISA ISHU YA SAIDO NA AMBUNDO KUSIMAMISHWA…MAYELE, SHABANI DJUMA WAJILIPUA YANGA…’WAMFESI’ NABI BILA UOGA..


IMEELEZWA kuwa, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amewatimua kambini wachezaji wawili wa kikosi hicho, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ na Dickson Ambundo.

Tukio hilo limetokea mara baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United uliochezwa Jumatatu wiki hii Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Yanga kwa sasa inajiandaa na mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Simba ambapo wanatarajiwa kucheza Mei 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Taarifa za uhakika kutoka Kambi ya Yanga iliyopo Shinyanga, zinasema kwamba, Kocha Nabi baada ya kugundua wachezaji hao kuondoka kambini bila ruhusa yake, aliamua kuwafukuza moja kwa moja na kuwataka kurudi kwao jambo ambalo ni wazi wataukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Simba.

“Ni kweli Saido na Ambundo wametimuliwa kambini na Kocha Nabi, hiyo ni baada ya kugundulika kuwa waliondoka kambini bila ruhusa yake.

“Hivyo sidhani kama watarejea na hii inaonekana mpaka pale ambapo timu itakaporejea Dar ndiyo wataweza kuungana na wenzao kambini.

“Baada ya tukio hilo, baadhi ya wachezaji wa Yanga akiwemo Fiston Mayele na Djuma Shabani, waliomba kwenda kuzungumza na Kocha Nabi ili awasamehe, lakini ilishindikana kwa kocha huyo kusimamia msimamo wake,” kilisema chanzo hicho.

SOMA NA HII  RASMI...KUELEKEA MSIMU UJAO WA LIGI YA MABINGWA AFRIKA...CAF WAIPA SIMBA HADHI SAWA NA AL AHLY YA MISRI...