Home Azam FC WATATU WA AZAM FC HATIHATI KUIKOSA TP MAZEMBE

WATATU WA AZAM FC HATIHATI KUIKOSA TP MAZEMBE


KESHO Azam FC kuna hatihati ya kuwakosa nyota watatu kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe kutokana na kutokuwa fiti kiafya.

 Frank Domayo, Agrey Morris na Salum Abubakar, ‘Sure Boy’ nyota wa Azam FC kuna hatihati ya kuukosa mchezo wa kesho dhidi ya TP Mazembe kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Azam chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina, kesho Februari 2 wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe, Uwanja wa Azam Complex.

Nyota wake wawili ambao ni Morris na  Sure Boy walipata majeraha kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC ambao ulichezwa Uwanja wa Azam FC na Azam FC ilishinda mabao 3-1.

Domayo bado hajaanza mazoezi na wachezaji wenzake kwa kuwa anasumbuliwa na majeraha.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa Domayo hajaanza mazoezi ila nyota wengine hali zao zinaendelea salama.

“Domayo bado hajaanza mazoezi kwa sasa ila Morris na Sure Boy hawa maendeleo yao ni mazuri kwa sasa ni suala la kusubiri na kuona,”.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF...KOCHA MFARANSA AWAPA MASHARTI HAYA AZAM FC...WAKISHINDWA IMEKULA KWAO...