Home news VIGOGO SIMBA WAVAMIA NYUMANI KWA KIBWANA SHOMARI..WAMWAGA AHADI ZA KUFA MTU ASISAINI...

VIGOGO SIMBA WAVAMIA NYUMANI KWA KIBWANA SHOMARI..WAMWAGA AHADI ZA KUFA MTU ASISAINI YANGA TENA…

IMEELEZWA kuwa vigogo watatu wa Simba wamevamia nyumbani kwa beki wa pembeni wa Yanga, Kibwana Shomari eneo la Bigwa wilaya ya Morogoro Mjini, kwa lengo la kuishawishi familia hiyo ili beki huyo asiongeze mkataba na Yanga kisha asaini Simba.

Kibwana alijiunga na Yanga Agosti 9, 2020 kwa mkataba wa miaka miwili ambapo kwa sasa anatumikia msimu wake wa mwisho katika
mkataba huo aliojiunga na Yanga akitokea Mtibwa Sugar.

Akizungumza na Gazeti la Championi Ijumaa, dada wa kwanza wa mchezaji huyo ambaye anafahamika kwa majina ya Zubeda Shomari, aliweka wazi kuwa uongozi wa Simba ulifika nyumbani kwao siku ya Jumanne ya Novemba 2 ambapo kubwa ambalo walilihitaji kutoka kwao ni kumshawishi beki huyo kutoongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Yanga ili wamsajili wao Simba.

“Ni kweli siku ya Jumanne viongozi wa Simba watatu ambao siwafahamu kwa majina yao walikuja na gari aina ya Prado nyumbani kwetu ambapo walinikuta mimi na mama yangu na walipojitambulisha kuwa ni viongozi wa Simba waliomba kuongea na mama yangu ambaye pia ni mama wa Kibwana Shomari.“

Walipomaliza kuongea na mama wakaondoka kisha mama akaniita akaniambia kila kitu huku kubwa zaidi walimuomba mama amshawishi Kibwana asiongeze mkataba wake wa kuendelea kuichezea Yanga kwa kuwa mkataba wake unakaribia kumalizika ndani ya Yanga.

“Na walimuambia kama atakubali kusaini Simba, wao watampatia mshahara mkubwa, watamjengea nyumba kubwa ya kifahari na kumnunulia gari kwa kuwa wao ni timu kubwa na yenye uhakika wa kushiriki michuano ya kimataifa,” alisema Zubeda Shomari.

Kibwana Shomari kwa sasa amekuwa katika kiwango bora ndani ya Yanga ambapo mara baada ya ujio wa beki Djuma Shabani ambaye anacheza katika nafasi ya beki wa kulia, Kibwana amehamishiwa upande wa kushoto ambapo amekuwa akicheza vizuri pia na kitendo ambacho kimesababisha aitwe kwenye timu ya taifa, Taifa Stars.

SOMA NA HII  USAJILI WA BIGIRIMANA YANGA WAMUIBUA NABI....AVUNJA UKIMYA NAMNA ALIVYOTAKA MAMBO YAWE...