Home Habar za Usajili Simba KUHUSU ISHU YA TETESI ZA PABLO KUFUKUZWA SIMBA…KUMBE MPANGO MZIMA UKO HIVI…TAMKO...

KUHUSU ISHU YA TETESI ZA PABLO KUFUKUZWA SIMBA…KUMBE MPANGO MZIMA UKO HIVI…TAMKO LATOKA..


HUKU ikiwa kwenye maandalizi makali kujiandaa mechi ya mwisho ya Kundi D, Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendamarie ya Niger Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, klabu ya Simba imewataka wanachama na mashabiki wake, kupuuza taarifa kuwa wapo mbioni kumfukuza …

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema kuwa taarifa hizo ni za kutungwa na zimeanzishwa makusudi na baadhi ya watu wasioitakia mema klabu hiyo, zikiwa na lengo la kupoteza utulivu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ahmed alisema kuwa ni kweli walimpa kocha huyo raia wa Hispania malengo ya kuifikisha nusu fainali, lakini hakuna sehemu yoyote waliyowahi kumwambia kuwa asipowafikisha watamtimua.

“Lengo la taarifa hizo za kutungwa ni kwa ajili ya kupoteza utulivu ndani ya klabu, hasa kuelekea kwenye pambano hilo muhimu. Ni kweli kocha tulimpa malengo ya kuifikisha timu nusu fainali, lakini hatukumwambia tusipofika tutamfukuza,” alisema.

“Ikitokea tukifika tutafurahi kwa sababu tumeweza kufikia malengo, lakini ikitokea tumekwama tutakaa chini na mwalimu tutamuuliza amekwama wapi atatuambia au atatupa sababu zake, na uongozi utakaa na kuzifanyia kazi, baada ya hapo maamuzi ya kimaslahi ya pande mbili yataamualiwa, lakini kwa sasa bado ni kocha wetu, hana wasiwasi na tunamuamini, ameleta mafanikio makubwa sana kwenye kikosi cha Simba kwa timu nzima na mchezaji mmoja mmoja, kuna sababu gani ya kumuwekea presha?” Alihoji Meneja huyo.

Alisema siku zote kwenye soka kocha anaweza asitimize malengo aliyowekewa, lakini viongozi wakawa na imani naye kwa sababu ya kuitengeneza timu imara, akaendelea kuwepo, lakini unaweza ukawa na kocha aliyetimiza malengo, lakini akafukuzwa kwa sababu kila mkiangalia viongozi mnaona hakuna muendelezo kwenye kikosi na hakuchezi vema.” alisema.

Simba inakwenda kucheza dhidi ya US Gendamarie kwenye mechi ambayo iwapo itashinda itakwenda moja kwa moja kwenye hatua ya robo fainali, huku kukiwa pia na tetesi zikizuka kuwa iwapo ikishindwa kufuza basi, ataonyeshwa mlango wa kutokea.

SOMA NA HII  WAKATI INONGA AKIPEWA TUZO YAKE LEO...AHMED ALLY ASHTUSHWA NA 'SAPRAIZI' YA MAMILIONI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here