Home Uncategorized HASHEEM IBWE AWAOMBA WATANZANIA WAENDELEE KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

HASHEEM IBWE AWAOMBA WATANZANIA WAENDELEE KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

HASHEEM Ibwe, mwandishi wa Habari za Michezo kutoka kituo cha Azam TV amesema kuwa kwa kipindi hiki ni muhimu kila mmoja kuchukua tahadhari kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona.

Ibwe ambaye amekuwa akikonga nyoyo za mashabiki wa Azam TV kutokana na mbwembwe zake akiwa anatangaza mechi huku ile swaga yake kwenye mechi ya Simba dhidi ya Yanga,”Kagere anatetema, sio mimi ni mguu” ikiwa ni miongoni mwa maneno yanayopendwa kutumiwa na mashabiki wake.

Pia kwa upande wa Yanga, mechi yake aliyotangaza dhidi ya Ndanda FC ambapo alisema kuwa ‘Tafsiri halisi ya Take Two’ ilijizolea umaarufu mkubwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ibwe amesema kuwa:”Ni muhimu kila mmoja kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kwani kwa sasa hali bado haijawa shwari na ugonjwa upo,”.  

SOMA NA HII  KOCHA YANGA : WACHEZAJI WALIKUWA WAMEINGIA KWENYE MFUMO