Home news HABARI NDIYO HIYO….METACHA , KAKOLANYA KUPISHANA MSIMBAZI…MCHONGO MZIKA UKO HIVI…

HABARI NDIYO HIYO….METACHA , KAKOLANYA KUPISHANA MSIMBAZI…MCHONGO MZIKA UKO HIVI…


HAKUNA siri tena. Unaambiwa mabosi wa Simba na Polisi Tanzania wapo hatua nzuri ya kubadilishana makipa, Metacha Mnata akiingia Msimbazi, huku Beno Kakolanya akitoka kwa Wekundu hao kwenda kwa maafande hao.

Mabosi wa Simba wanadaiwa wanaisaka saini ya Metacha aliyewahi kuzidakia Mbao, Azam na Yanga, ili atue Msimbazi kumpa ushindani wa kweli kipa namba moja wao, Aishi Manula, lakini maafande hao wakitoa masharti ya kutaka kupewa Kakolanya ambaye anasugua benchi kwa sasa.

Ipo hivi. Uongozi wa Polisi umethibitisha kuwa Simba imewafuata kumtaka Metacha na wao wakatoa sharti kwamba endapo watamuuza kipa huyo basi na wao wanamtaka Kakolanya katika kikosi chao ili mambo yao yaendelee vizuri kama ilivyo sasa kwenye Ligi Kuu Bara.

Mwenyekiti wa Polisi Tanzania, Kamishna wa Polisi, Charles Mkumbo alisema ni kweli wamepokea ofa hiyo na makubaliano yao bado hayajakamilika ila sharti walilolitoa ni hilo la kupewa Kakolanya ili azibe pengo la Metacha kama atatua Msimbazi.

“Bado tunahitaji huduma yake kutokana na anachokifanya ila kama yeye mwenyewe ataridhia kwenda hatutakuwa na pingamizi, tutafanya biashara na tutataka kumchukua Kakolanya kama mbadala,” alisema Mkumbo na kuongeza;

“Hakuna timu ambayo inamng’ang’ania mchezaji kama makubaliano yatafikia muafaka kila upande unatakiwa kuridhia kwa kile kitakachozungumzwa ili mambo mengine yaweze kuendelea,” alisema.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo aliweka wazi, dirisha hili la usajili wanatafuta mshambuliaji mmoja ili aweze kumuongezea nguvu Vitalis Mayanga ambaye ndiye kinara wa upachikaji mabao kwenye timu hiyo.

“Tuna mshambuliaji mmoja mzuri na ametuthibitishia kwa kuonyesha ubora tunahitaji msaidizi wake katika dirisha hili.”

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUFUNGA GOLI JUZI..MAKAMBO BADO 'ANAWENGE '..AWATAJA SIMBA SC