Home news YANGA KUMEKUCHA…WAZIDI KUMIMINA MIZAWADI YA ‘KRISMASI BOXING DAY’..SAFARI HII KICHEKO TU..

YANGA KUMEKUCHA…WAZIDI KUMIMINA MIZAWADI YA ‘KRISMASI BOXING DAY’..SAFARI HII KICHEKO TU..


WAKATI watu wakiwa bize na siku ya zawadi za sikukuu ya christmas ‘Boxing Day’ Yanga imewapa mashabiki zake ya ushindi dhidi ya Biashara United.

Ilikuwa katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyomalizika dakika  chache zilizopita kwenye Uwanja wa Benjain Mkapa baina ya timu hizo mbili na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Biashara ndiyo ilianza kupata bao dakika ya pili kupitia kwa Atupele Green kabla ya dakika ya 40, mshambuliaji Fiston Mayele kuisawazishia Yanga na kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko Katika nyakati tofauti, Yanga ikiwatoa Bryson David,  Fiston Mayele na Djuma Shabaa na kuingia Bakari Mwamnyeto, Yassin Mustapha na Herritier Makambo.

Kwa upande wa Biashara walitoka Atupele, Methew Tayo na Abdulmajid Mangalo na nafasi zao kuchukuliwa na Christian Zigah,  Opare Collins na Salum Kipaga.

Mabadiliko hayo yaliipa zaidi nguvu Yanga ambayo dakika ya 79 ilipata bao la pili kupitia kwa Said Ntimbazonkiza kwa mkwaju wa Penalti baada ya Jesus Moloko kuchezewa madhambi ndani ya boksi la Biashara.

Ushindi huo umeifanya Yanga kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wa ligi hadi sasa ikiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi 10 ikishinda nane na sare mbili ikikusanya pointi 26.

Baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika wachezaji na Benchi la ufundi la Yanga waliingia Uwanjani na kuwapungia mikono mashabiki wao kama ishara ya kuwashukuru.

SOMA NA HII  FT: HAYA HAPA MATOKEO YOTE YA MECHI ZA LEO....MAYELE NA NTIBAZONKIZA WAGAWANA TUZO...