Home Uncategorized THOMAS PARTEY KUIBUKIA ARSENAL MSIMU UJAO

THOMAS PARTEY KUIBUKIA ARSENAL MSIMU UJAO


THOMAS Teye Partey, nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Atletico Madrid inayoshiriki La Liga inaripotiwa kuwa msimu ujao atajiunga na Klabu ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England. 
Kiungo huyo mwenye miaka 26 raia wa Ghana amejiunga na Atletico msimu wa 2015 mpaka sasa amecheza jumla ya mechi 118 akitupia mabao 11.

Nyota huyu ambaye ni raia wa Ghana kwa sasa inaelezwa kuwa Arsenal wanaiwinda saini yake kwa ukaribu huku dalili zikionesha kuwa atatua kwa washika bunduki hao.
Ripoti zinaeleza kuwa kwa sasa amebakiza hatua za mwisho kujiunga na Arsenal inayotumia Uwanja wa Emirates kwa mechi zake za nyumbani baada ya  dau la Euro milioni 43 kuelezwa kuwa limewekwa meazani na mabosi wa Arsenal.
Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta inaelezwa kuwa ndiye ambaye amependekeza kumpata kiungo huyo ili akaongeze nguvu msimu ujao ndani ya kikosi chake ambacho kwa sasa kipo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

SOMA NA HII  SIMBA MAJANGA TUPU NYOTA WATANO KIKOSI CHA KWANZA OUT