Home news BAADA YA KUTEMANA NA YANGA, CARLINHOS HUYU HAPA NA TIMU YAKE MPYA..

BAADA YA KUTEMANA NA YANGA, CARLINHOS HUYU HAPA NA TIMU YAKE MPYA..


ALIYEKUWA kiungo mshambuliaji wa Yanga Carlos Carlinhos ametua kwa mabingwa wa Angola Sagrada Esperanca kwa uhamisho huru.

Nyota huyo ambaye alikuwa ni kipenzi cha Yanga amerejea kwao nchini Angola baada ya kuvunja mkataba na Yanga kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Sababu za kuondoka kwa nyota zilielezwa kuwa alidai anapata changamoto ya chakula hivyo Uongozi wa Yanga umsafirishe mkewe aje Tanzania la sivyo angevunja mkataba jambo ambalo uongozi wa Yanga walishindwa kulifanya na kuamua kuvunja nae mkataba.

Aidha Carlinhos alishinikiza uongozi wa Yanga kuvunja mkataba licha ya Yanga kuendelea kuonyesha imani kwake na mchezaji huyo hali iliyomfanya kuanza kusumbua kinidhamu kwa Kupenda kujitenga na kutaka huduma ‘spesho’ tofauti na wachezaji wenzake wanapokuwa kambini hali iliyomuondoa nchini.

SOMA NA HII  KISA MAKOSA YA KINIDHAMU...GOMES ACHUKUA MAAMUZI HAYA KUHUSU JONAS MKUDE