Home Simba SC SIMBA YAMPELEKA GYM SMSHAMBULIAJI WAKE MPYA

SIMBA YAMPELEKA GYM SMSHAMBULIAJI WAKE MPYA


BAADA ya kukamilisha usajili wa kujiunga na Simba, aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya City, Kibu Denis, ameanza programu maalum ya mazoezi ya gym kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea msimu ujao wa 2021/22.


Inaelezwa kuwa, tayari Kibu 
amekamilisha kila kitu na Simba kwa ajili ya kuwatumikia msimu ujao, na sasa anasubiri kutambulishwa rasmi kama ambavyo wachezaji wengine wapya wa kikosi hicho walivyofanyiwa.

 

Kibu amesajiliwa Simba kama pendekezo la Kocha Mkuu, Didier Gomes ambapo anakuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, ambayo inatajwa iko kwenye mpango wa kuachana na straika mmoja.

 

Akiwa na Mbeya City msimu uliopita, Kibu alionesha uwezo alifunga mabao sita na kupata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi, Juni, mwaka huu.


Kuhusu usajili wake, Kibu aliliambia Spoti Xtra kwamba: â€śNipo Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha usajili wangu kwenye klabu moja kubwa, tuendelee kusubiri kila kitu kitawekwa wazi,” .

SOMA NA HII  MWENDO WA MANULA, UNAZUNGUMZA KWA SAUTI YA JUU SANA