Home Habari za michezo KUHUSU NAMBA 6 MPYA WA YANGA…ALLY KAMWE AANIKA A-Z DILI LILIVYO….

KUHUSU NAMBA 6 MPYA WA YANGA…ALLY KAMWE AANIKA A-Z DILI LILIVYO….

Tetesi za Usajili Yanga

Wakati wengi wakiendelea kubashiri mrithi wa jezi ya Kiungo Feisal Salum alietimkia Azam FC.

Afisa habari wa Yanga Ally Kamwe ameibuka na kuwataka watu waache kujiumiza vichwa kwani hakuna mtu anaemjua mchezaji huyo zaidi ya watu watano tu ambao wanatoka Klabu ya Yanga.

Akizungumza Ally Kamwe anasema;

“ Namba sita hajulikani ,tunamjua watu watano Yanga nzima , hii ndio uone Yanga stori zetu huwa hazivuji lakini wenzetu picha kibao , Sisi utaona tu kwenye magazeti Yanga mpya lakini hujui Yanga ipi ?

Yanga inatajwa kumalizana na Zougrana Mohamed ambaye ni kiungo kutoka ASEC Mimosas, huku ikifanya mazungumzo ya kumuogezea mkataba mshambuliaji Fiston Mayele aliyeibuka mfungaji bora baada ya kutupia mabao 17 msimu wa 2022/23.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ameweka wazi kuwa wakati wa usajili wataingia sokoni kwa umakini kuwaongeza wachezaji bora, watakaoongeza ushindani kwenye timu hiyo kwa mbinu ya kipekee.

“Inapofika suala la usajili inajulikana namna ambavyo huwa tunafanya kazi na ambacho kinatokea tunapokuwa tunahitaji mchezaji baada ya kumfuatilia kwa umakini jina likifika hapa kazi imekwisha.

“Wanajua shughuli ambazo huwa tunafanya tumefanikisha usajili wa wachezaji wengi na hizo ni kazi ambazo ninazimudu, hivyo hakuna ambacho kitashindikana,” alisema Hersi.

SOMA NA HII  STAA YANGA:- PACOME ANATUMIA NGUVU NYINGI...CHAMA ANATUMIA AKILI NYINGI...ANAMCHAMBUA HADI KIPA