Habari za Simba leo
Habari za Simba Leo

BREAKING NEWS…LAMECK LAWI ARUDI NCHINI…AJIFICHA HOTELINI

Abubakar August 19, 2024 2:28 pm

BAADA ya usajili wake kuzua balaa na mgogoro mkubwa sana kati ya Simba na Coastal Union, baadae Kijana akaenda zake Ulaya kujaribu bahati yake na kuangalia kama atapata maisha.

Inaelezwa kwamba Lameck Elias Lawi tayari amerudi nchini juzi na yupo kwenye Hotel moja pale Magomeni (Jina tumelihifadhi) baada ya majaribio yake ulaya.

Lawi anategemea nusra ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kumpeleka Simba au Coastal maana shauri lake lipo kwao japo waliziambia timu hizi zikae na zikubaliane zenyewe.

Wakati Simba ikitambulisha wachezaji wake wapya kwa msimu wa 2024/25, jina la Lawi halikuwa sehemu ya majina yaliyotambulishwa siku ya Simba Day.

Kwa upande wa Coastal Union wao waliendelea kubaki na msimamo wao wa kwamba, Lawi ni mchezaji wao halali Simba walienda kinyume na makubaliano waliyowekeana.

GAMONDI AMTAJA CHAMA…ANA KAZI NAE FADLU DAVIDS AANZA NA VIHUNZI HIVI