Israel Mwenda Yanga
Yanga SC

Yanga Yafunguka Sakata la Israel Mwenda: Upangaji Matokeo Wakanushwa

Vardo August 19, 2026 2:49 pm

Uongozi wa klabu ya Yanga SC hatimaye umevunja ukimya na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusiana na sintofahamu inayomkabili beki wao wa kulia, Israel Patrick Mwenda, huku wakikanusha vikali taarifa zinazomhusisha mchezaji huyo na tuhuma za upangaji wa matokeo.

Akizungumza hivi karibuni kwenye mahojiano maalum kupitia kipindi cha michezo cha Crown FM, Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, alibainisha kuwa klabu hiyo haina taarifa za mahali alipo mchezaji huyo kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Kutoweka Klabuni na Barua ya Mwenda Kamwe alieleza kuwa Mwenda alikuwa amewasilisha barua rasmi kwa uongozi akiomba kupewa muda wa kujitenga na timu kutokana na changamoto za kisaikolojia zilizokuwa zikimsumbua. Hata hivyo, tangu kuwasilishwa kwa barua hiyo, mchezaji huyo hajarejea kambini wala kutoa taarifa yoyote ya msingi kuhusu kurejea kwake.

“Mchezaji huyu haonekani klabuni kwa mwezi na siku kadhaa bila sababu ya msingi. Aliandika barua akiomba kujitenga na timu kutokana na matatizo ya kisaikolojia, lakini mpaka sasa hatujui alipo,” alisema Kamwe.

Ufafanuzi huo unakuja kufuatia kauli za baba mzazi wa mchezaji huyo zilizoibua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo uongozi wa Wananchi umesema limewashangaza kwa kuwa hata wao hawana mawasiliano ya moja kwa moja na Mwenda.

Yanga Yakanusha Tuhuma za Upangaji Matokeo Kuhusu uvumi ulioenea kuwa klabu hiyo ilikuwa ikimshutumu Mwenda kuhusika na vitendo vya upangaji matokeo (match-fixing), Kamwe alipuuza madai hayo na kusisitiza kuwa Yanga haijawahi kumtuhumu au kumhusisha mchezaji huyo na suala lolote la kimaadili au kihalifu.

Sababu za Kutotambulishwa Siku ya Wananchi Akitolea ufafanuzi sababu za mchezaji huyo kutotambulishwa wakati wa tamasha la Siku ya Wananchi, Msemaji huyo alieleza kuwa isingekuwa na mantiki kumtambulisha mchezaji ambaye hajajiunga na wenzake na wala klabu haijui alipo.

Sakata hili linaendelea kuibua maswali mengi miongoni mwa mashabiki wa Yanga, huku uongozi ukisubiri mchezaji huyo kurejea ili kutoa maelezo ya kina kabla ya kuchukua hatua za kifani au kisheria.

Eastern Fury Imewasili Na Nafasi Mpya ya Nguvu Na Ushindi Yanga vs Coastal Union: Mngqithi Afichua Mipango Mizito na Tahadhari Kibarua cha KMC