Azam FC vs Coastal Union
Azam FC

Mastaa 6 Azam FC Wawasili! Kuisambaratisha Coastal Union Ligi Kuu NBC?

Vardo October 7, 2026 9:38 am

Kikosi cha Azam FC kimepata nguvu mpya baada ya mastaa wake sita waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) nchini Morocco kurejea rasmi kambini na kuanza mazoezi makali kuelekea mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union.

Wachezaji hao wameungana na wenzao mara baada ya kukamilisha majukumu ya kitaifa, huku benchi la ufundi chini ya kocha mkuu likiongeza kasi ya maandalizi kabla ya kuwakabili Wagosi wa Kaya katika mchezo unaotarajiwa kupigwa Ijumaa, Oktoba 9, 2026.

Kupitia kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii, Azam FC imethibitisha kurejea kwa nyota hao:

“Wachezaji wetu sita waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, wamejiunga rasmi mazoezini na wachezaji wenzao, kujiandaa na mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya Coastal Union,” ilieleza taarifa ya klabu hiyo.

Majina ya Mastaa Waliorejea Kambini Azam FC:

  1. Feisal Salum ‘Feitoto’

  2. Lameck Lawi

  3. Pascal Msindo

  4. Nassor Saadun

  5. Himid Mao

  6. Abdul Suleiman ‘Sopu’

Kurejea kwa wachezaji hawa kunampa kocha wa Azam FC wigo mpana wa kikosi chake kutokana na uzoefu na ubora wa kila mmoja wao. Azam FC inalenga kupata alama tatu muhimu ili kuendeleza wimbi la ushindi na kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Sasa nguvu na akili zote za wana-lambalamba zimeelekezwa kwa Coastal Union, huku benchi la ufundi likitumia siku chache zilizobaki kuweka mbinu za mwisho zitakazohakikisha wanainuka na ushindi siku ya mchezo.

Siri ya Mafanikio ya Peter Shalulile Yanga SC: Nidhamu na Imani Nje ya Uwanja Mtego wa Nje: Siri za Mabondia wa Tanzania Kuteseka Ugenini na Jinsi ya Kujinasua