Simba vs Yanga Uwanja wa Uhuru
Simba SC

Ahmed Ally Afunguka: Utata wa Majeraha ya Libasse Gueye na Maandalizi ya Dabi ya Kariakoo Uwanja wa Uhuru

Vardo October 7, 2026 9:25 am

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ametoa taarifa rasmi kuhusu kurejea kwa kikosi hicho nchini kikitokea Afrika Kusini, huku akikanusha vikali uvumi wa majeraha wa mshambuliaji wao hatari, Libasse Gueye.

Simba imekuwa nchini Afrika Kusini kuweka kambi fupi ya kujiandaa na mechi zinazofuata, na sasa wamerejea nchini wakiwa kamili kuelekea mchezo wao unaosubiriwa kwa hamu mkubwa dhidi ya watani wao wa jadi.

Hali ya Kikosi na Taarifa za Libasse Gueye

Akizungumzia maandalizi ya timu hiyo, Ahmed Ally ameeleza kuwa wachezaji wote walipata fursa ya kufanya mazoezi ya pamoja kulingana na ratiba zao za kujiunga na kambi.

“Wachezaji wetu wote ambao hawakuwa na majukumu ya timu ya taifa waliwasili kambini Afrika Kusini kwa nyakati tofauti, lakini wote walipata muda wa kufanya mazoezi na wenzao na wote wamerejea salama nchini Tanzania,” amesema Ahmed Ally.

Kuhusu taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa mshambuliaji Libasse Gueye amepata majeraha, Ahmed Ally amezipuuzia taarifa hizo na kuzitaja kuwa ni mbinu za kutengeneza taharuki.

“Ziko fununu nyingi kuhusu Libasse Gueye kwamba ameumia. Ni watu tu wanataka kuleta taharuki kwa mashabiki wa Simba. Niwaambie tu kwamba Libasse yuko salama kabisa, hajaumia hata kucha na yuko tayari kwa ajili ya mapambano ya mwezi huu wa Oktoba,” alisisitiza.

Dabi ya Kariakoo Kutimua Vumbi Uwanja wa Uhuru

Mbali na kueleza hali ya kikosi, Ahmed Ally amethibitisha kuwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga SC utapigwa wiki hii katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mchanganuo wa Mchezo:

  • Mechi: Simba SC vs Yanga SC

  • Tarehe: Oktoba 10, 2026 (Jumamosi)

  • Uwanja: Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam

  • Muda: Saa 1:00 Usiku

Ahmed amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao katika pambano hilo linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Tanzania U-23 Yaondolewa AFCON U-23 Licha ya Kuisambaratisha Kenya 3-1 Uhuru Siri ya Mafanikio ya Peter Shalulile Yanga SC: Nidhamu na Imani Nje ya Uwanja