Habari za Yanga Leo
HAJI MANARA AONDOSHWA YANGA…ALI KAMWE NI BOSI
Abubakar
August 22, 2024
1:05 pm
Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said amesema Ally Kamwe ndiye Afisa Habari wa Yanga SC, na Haji Manara ni mwanachama ambaye anatafutiwa nafasi atakayoweza kuhudumu klabuni hapo.
Kupitia kipindi cha Jana na Leo cha Wasafi Media, Eng. Hersi Said amesema; “Kwa mujibu wa katiba yetu, mimi ndiye msemaji mkuu wa klabu, ikitokea nina majukumu mengine, nita-delegate power kwa mtu mwingine. Yanga hatuna Bosi wa Idara ya Habari tuna Afisa Habari huyo ndiye kiongozi kwenye Idara ya Habari ambaye ni Ally Kamwe.
“Manara ni mwanachama wa Yanga, ambaye alikuwa msemaji wa Yanga, amemaliza adhabu yake aliyopewa na TFF, amerejea tumempokea kama mtumishi wa klabu, tunaangalia nafasi ya kumpa aendelee kutekeleza majukumu yake,” amesema Eng. Hersi Said.
Baada ya kumaliza adhabu yake Manara alionekana kama kurudi kwenye nafasi yake, hadi kufanya hamasa za Kilele y Wiki ya Wananchi, na kwenye Utambulisho wa Wachezaji alihusika vizuri.
Alivyomaliza tukio hilo Haji Manara hajawahi kuonekana kwenye tukio lolote la Yanga.