Habari za Simba, Ahmed Ally
Habari za Simba Leo

SIMBA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI WIKIENDI HII

admin September 3, 2024 12:22 pm

KLABU ya Simba inatarajia kucheza mechi ya kirafiki wikiendi hii kabla ya kusafiri kwenda Libya kucheza mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahli Tripoli.

Kwa mujibu wa Meridanbet Sports, Ahmed Ally amesema kuwa inawezekana mchezo huo ukawa dhidi ya timu ya Ligi Kuu au Ligi Daraja la Kwanza ambapo kesho Jumatano watasema watacheza na nani.

“Tunaendelea na mazoezi kama kawaida kujiandaa na safari ya kwenda Libya kucheza mechi yetu ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya.

“Lakini kabla ya hapo Wikiendi hii tutacheza mechi ya kirafiki na timu ambayo tutawatangazia kesho au Kesho Kutwa Jumatano

RAIS SAMIA AMWAGA MAMILION TAIFA STARS…SIMBA, YANGA NA AZAM WAUNGANA MWENDA AFUNGUKA SAKATA LAKE…NINA HELA YA KUTUMIA..WAMEVUNJA MAKUBALIANO