Home Habari za Simba Leo LEONEL ATEBA AKALISHWA CHINI SIMBA

LEONEL ATEBA AKALISHWA CHINI SIMBA

HABARI ZA SIMBA-ATEBA

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema licha ya mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Leonel Ateba kufunga bao moja katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal ya Sudan, bado anapaswa kuendelea kupambana zaidi kikosini.

Nyota huyo raia wa Cameroon alifunga bao hilo ikiwa ni mchezo wa kwanza kwake akiwa na kikosi hicho tangu ajiunge msimu huu na kuifanya Simba itoke sare ya 1-1 katika mechi kali na ya kusisimua iliyopigwa juzi kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge.

Akizungumza kuhusu mwanzo mzuri wa Ateba ndani ya Simba Baada ya kufunga juzi dhidi ya Al HILAL, Fadlu bado hajataka kusema kuwa nyota huyo ndiyo atakuwa chaguo la kwanza kwenye eneo la ushambuliaji.

“Hakuna Mchezaji mwenye uhakika wa kuanza kwenye kikosi Cha kwanza hadi Sasa. Hongera Kwa Ateba alitimiza jukumu lake juzi, lakini anatakiwa afanye kazi Kweli kama anataka kucheza,” alisema.

SOMA NA HII  BAADA YA SAKATA LA 'SUB' YA CHAMA...MBRAZILI SIMBA AIBUKA NA 'SOLUSHENI' HII...