Home Habari za Simba Leo FADLU DAVIDS HATAKI KULALA…AMTAKA ATEBA KUFANYA JAMBO LEO

FADLU DAVIDS HATAKI KULALA…AMTAKA ATEBA KUFANYA JAMBO LEO

HABARI ZA SIMBA- FADLU

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho Afrika klabu ya Simba inaikaribisha klabu ya Al Hilal ya Sudan katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Hata hivyo, katika mchezo huo huenda Simba ikamtambulisha straika wake mpya, Leonel Ateba, ambaye alikuwa nyota wa mwisho wa kimataifa kusajiliwa.

Ateba, hajaonekana katika michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo Wekundu wa Msimbazi wamecheza dhidi ya Tabora United na Fountain Gate kutokana na kukosekana kwa vibali.

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, amewaambia mashabiki wa timu hiyo leo itakuwa ni nafasi nzuri kumwona mchezaji huyo kwa mara ya kwanza kwa sababu atamtumia, huku pia akiendelea kumpa nafasi straika wa Mtanzania, Velentino Mashaka, ameshapachika mabao mawili.

Fadlu alisema Mashaka ameanza kumpa mwangaza mzuri na anaamini ataendelea kuwa ‘moto’.

“Ateba kesho (leo) ndiyo atakayeongoza mashambulizi kwa sababu nataka nimwone kwa uzuri zaidi katika mchezo mkubwa kama huu, nadhani na mashabiki nao watapata fursa ya kumwona baada ya kukosekana mara mbili, lakini pia kuna Valentino, naye atapata nafasi, ni kijana mzuri ambaye katika mechi zote mbili amefunga bao moja akitokea benchi. Mukwala naye itategemea kama akichelewa kwenda katika kikosi cha taifa atacheza, lakini kama akiondoka mapema hatakuwepo,” alisema Fadlu.

Aliongeza pia atatumia mechi hiyo kuwapa nafasi wachezaji wengine ambao hawakutumika kabisa kwenye mechi mbili za Ligi Kuu walizocheza ili wawe na utimamu wa mwili vizuri.

Simba itaanza kutupa karata yake katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ugenini Septemba 13, mwaka huu dhidi ya Al Ahly Tripoli huku mchezo wa marudiano utafanyika wiki moja baadaye kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

SOMA NA HII  YANGA YASHTUKIA DILI LA USAJILI...INJINIA NA GAMONDI WAKAA KIKAO