Home Habari za Yanga Leo YANGA YASHTUKIA DILI LA USAJILI…INJINIA NA GAMONDI WAKAA KIKAO

YANGA YASHTUKIA DILI LA USAJILI…INJINIA NA GAMONDI WAKAA KIKAO

Injinia Hersi Rais wa Yanga SC

YANGA wameamua kurudi nyuma kwanza kuangalia kuna ulazima gani wa kusajili kiungo mkabaji mzawa ikiwa kuna uwezekano wa kuendelea kubaki na Jonas Mkude na Zawadi Mauya ambao watashirikiana vema na Khalid Aucho raia wa Uganda.

Wakakubaliana na wazo la Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kwamba wanaweza kusubiri dirisha kubwa lipite na kutumia kipindi hiki kutafuta mtu sahihi kabla ya kufika dirisha dogo, Desemba mwaka huu ambapo ndipo wafanye jambo.

Awali Yanga walikuwa na mipango ya kutafuta mbadala wa Khaled Aucho ambaye, pindi anapokosekana kwenye kikosi hicho, kunakosa utulivu.

Safu ya kiungo ya Yanga kwa sasa inaundwa na Khaled Aucho, Jonas Mkude, Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoa, Zawadi Mauya, Mudathir Yahya, Aziz Ki, na Salum Abubakar.

Ni moja ya safu bora na tishio kwa sasa TANZANIA, lakini anayeibeba safu ya ulizni wa Yanga, ni Khaled Aucho na Jonas Mkude, huku safu ya ushambuliaji ikibebwa na Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya, Pacome, Aziz Ki, Salum Abubakar Sure Boy.

Rais wa Yanga Injinia Hersi alinukuliwa akisema kwamba, msimu ujao timu hiyo itafanya usajili wa maana, ili kukiongezea kiwango na ushindano kikosi hicho.

Yanga itakipiga msimu ujao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku  watani zao Simba wakitupwa kwenye kombe la shirikisho Afrika, ikiwa ni anguko kwao.

SOMA NA HII  MZIZE HAJAWAHI KUFUNGA MABAO YA KUIBEBA TIMU...OSCAR OSCAR