Home Habari za Simba Leo MO DEWJI AMKATAA LOMALISA…AANZA NA LAKRED

MO DEWJI AMKATAA LOMALISA…AANZA NA LAKRED

HABARI ZA SIMBA

MWEKEZAJI wa klabu ya Simba Mohammed Dewji, amezuia uwezekano wa beki Joyce Lomalisa kutua Msimbazi lakini amemuita kipa Ayoub Lakred kwa ajili ya mazungumzo nyumbani kwake nchini Dubai.

Habari za uhakika ambazo tunazo ni kwamba Ayoub ambaye mkataba wake na Simba umemalizika amewaambia viongozi wa Simba kwamba ana ofa mbili kutoka klabu ya Pyramids na Zamalek zote za Misri.

Lakini tunafahamu kwamba kipaumbele kwa Mmorocco huyo ni kuendelea kucheza akiwa na Simba, kwani mazingira na mapokeo ya mashabiki ameyapenda.

Lakini kuna changamoto mbili ambazo zinaweza kumfanya Lakred aondoke au asalie Simba kwa msimu ujao.

Moja nafasi kubwa ya kubakia Simba itategemea pia nafasi ya kocha wa makipa wa klabu hiyo Dani Cadena kama ataendelea kuwa sehemu ya benchi la Simba msimu uajo.

Pili, Familia yake, yaani mkewe ambaye alimpa taarifa za yeye Ayoub Lakred kuhitaji kubaki Tanzania, hivyo aje kuangalia mazingira na hali ya hewa kama atayapenda waishi wote hapa Tanzania akitumikia mkataba wake.

Sasa suala la usajili wake limefika mezani kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na muwekezaji wa klabu ya Simba Mo Dewji, ambaye ndiye aliyemleta klabuni hapo.

Kwahyo Mohamed Dewji ameshikilia hatma ya nyanda huyo, ambaye alikuwa na msimu mzuri tangu atue Simba, lakini awali alianza vibaya.

SOMA NA HII  MGUNDA:- MECHI NA JKT NI SAWA NA KUFUNGA SHULE TU...HATMA YETU ITAJULIKANA HAPO....