Home Habari za Yanga Leo YANGA KUTENGENEZEWA PESA YAO…MWIGULU NCHEMBA ASHAURI

YANGA KUTENGENEZEWA PESA YAO…MWIGULU NCHEMBA ASHAURI

tetesi za usajili Yanga leo

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema kwa mafanikio ambayo timu ya Yanga imeyapata anatamani kumshauri Gavana wa Benki Kuu (BoT) kuweka nembo ya klabu hiyo kama kungekuwa na noti ya Sh100 kuyaenzi mafanikio hayo.

Dk Mwigulu ametumia sehemu ya hotuba yake ya uwasilishaji wa Bajeti ya Serikali 2024/25 ya Sh49.3 trilioni jana Alhamisi, Juni 13, 2024 akizipongeza timu za Azam, Coastal Union, Simba na Yanga kwa kufanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Kimataifa.

Yanga na Azam zitacheza Klabu Bingwa Afrika huku Simba na Coastal wakicheza Kombe la Shirikisho. Ikiwa ni mara ya kwanza kwa Simba kuangukia huko kwa miaka ya hivi karibuni.

Simba ilikuwa ndiyo Baba wa michuano ya Mabingwa Afrika kwa nchi za Tanzania,  lakini kwa msimu uliomalizika klabu hiyo haikuwa na ubora mkubwa kiushindani ndani ya uwanja, hali iliyosababisha Mnyama kumaliza ligi akiwa nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC na Yanga.

“Kwa umaalum kabisa nimpongeze GSM kwa uwekezaji mzuri alioufanya ambao umebadilisha kabisa taswira na uwezo wa kiuchezaji wa timu ya Yanga. Mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mzuri uliofanywa na GSM. GSM wewe ni mwamba, ujengewe sanam/mnara pale Makao Makuu ya Yanga,” alisema Dk Mwigulu.

Klabu ya Yanga ni mabingwa wa Ligi  Kuu kwa mara ya tatu mfululizo, huku wakitwaa taji hilo mara  30.

SOMA NA HII  JOB AWACHANA MASTAA YANGA..."ACHENI DHARAU AISEE...ISHU NZIMA IKO HIVI