Home Habari za Simba VAR KUTUMIKA LIGI KUU MSIMU UJAO, SIMBA…YANGA ZAJIPANGA

VAR KUTUMIKA LIGI KUU MSIMU UJAO, SIMBA…YANGA ZAJIPANGA

habari za yanga-VAR

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, viwanja vitakavyotumika kwa michuano hiyo vitafungwa teknolojia inayomsaidia mwamuzi kufanya marejeo ya picha (Video Assistance Referee-VAR) kwa ajili ya kuhakikisha matokeo yanayopatikana yanakuwa ya haki.

Mwigulu amesema katika kuhakikisha hilo linafanikiwa, Serikali inakusudia kuwasilisha pendekezo la kuondoa kodi kwenye vifaa vinavyotumika kwenye teknolojia hiyo kuanzia mwaka mpya wa fedha 2024/2025.

Dk Mwigulu ameyasema hayo Alhamisi, Juni 13, 2024 wakati akisoma bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka mpya wa fedha 2024/2025.

“Tunataka matokeo yawe ya haki, sio kuna timu msimu unaisha imepewa penalti zaidi ya 10 na wengine mabao yao yanakataliwa, hivyo msimu ujao tunakwenda kutumia VAR,” amesema Dk Mwigulu.

Ikumbukwe kwamba viwanja vinavyoweza kufungwa VAR kwa aajili ya mashindano ya Ligi Kuu Bara, ni Uwanja wa Benjamin Mkapa,Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Uwanja wa KMC Mwenge kama utakamilika, uwanja wa Kaitaba Kagera na uwanja wa Mkwakwani Tanga, Uwanja wa Ruangwa Lindi.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa ligi kuu kutumia teknolojia hiyo ghali zaidi kwa sasa duniani, na Tanzania itakuwa ndiyo nchi ya  kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati kuanza kutumia VAR kwenye mechi zake.

Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa Simba na Yanga zimewahi kuhukumiwa vibaya na VAR, kwa nyakati tofauti, Simba waliadhibiwa na Orlando Pirates hatua ya robo fainali ya pili huko Afrika ya kusini kwa goli lilifungwa hali ya kuwa mchezaji alikuwa ameotea.

Yanga SC walihukumiwa juzi tu hivi, wakiwa Afrika Kusini dhidi ya Mamelodi  Sundowns haua ya robo fainali CAFCL, bao halali la Aziz Ki lilikataliwa.

SOMA NA HII  ROBERTINHO ASEMA HAYA KUHUSU ONANA, NGOMA SIMBA HAPAKALIKI TENA