Home Uncategorized ISHU YA YANGA KUIKIMBIA SIMBA KIJANJA MAPINDUZI CUP IPO HIVI

ISHU YA YANGA KUIKIMBIA SIMBA KIJANJA MAPINDUZI CUP IPO HIVI


KUTOKANA na mashabiki wa Yanga kukasirika kitendo cha Yanga kupoteza mchezo wao wa nusu fainali kwenye Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar huku ikielezwa kuwa ni ujanja wa kuikimbia Simba uongozi wa Yanga umesema kuwa hakuna kitu kama hicho.

Yanga ilianza kufunga bao la kuongoza kwenye mchezo huo kupitika kwa Deus Kaseke jana Uwanja wa Amaan lilisawazishwa na Mtibwa Sugar dakika ya 90+2 na Shomari Kibwana na kupelekea kufungwa kwa penalti 4-2.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa hawaiogopi timu yoyote ni upepo tu haukuwa kwao jana.

“Tunacheza kwa malengo, wachezaji wamepambana kwa hali na mali mwisho wa siku tumefungwa usiku kutokana na makosa ya wachezaji wetu na bahati kuwa kwa Mtibwa Sugar.

“Upande wa penalti hazina mwenyewe tunarudi Bongo kujiaandaa na ligi, kuna mengi ya kufanya mashabiki watupe sapoti na hatujawakimbia Simba sisi,” amesema.

Yanga wamerejea leo Bongo wakitokea Visiwani Zanzibar na wamewaacha wababe wao Mtibwa Sugar wakisubiri mshindi wa pili kati ya Azam ama Simba ili wacheze nao fainali, Januari 13.

SOMA NA HII  KIUNGO MSHAMBULIAJI WA SIMBA ALIYEWEKWA KWENYE RADA ZA NAMUNGO ANATIMIZA MIAKA KADHAA