Home Uncategorized KIUNGO MSHAMBULIAJI WA SIMBA ALIYEWEKWA KWENYE RADA ZA NAMUNGO ANATIMIZA MIAKA KADHAA

KIUNGO MSHAMBULIAJI WA SIMBA ALIYEWEKWA KWENYE RADA ZA NAMUNGO ANATIMIZA MIAKA KADHAA

 


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Miraji Athuman ambaye anatajwa kuwekwa kwenye rada za mabosi wa Namungo leo Desemba 27 anatimiza miaka 27 ya kuletwa duniani.


Msimu huu wa 2020/21 mambo yamekuwa magumu kwake kupata namba kikosi cha kwanza tofauti na msimu uliopita ambapo alikuwa na nafasi kikosi cha kwanza.


2019/20 alitupia mabao 7 na kutoa pasi moja ya bao majeraha ya mara kwa mara ni moja ya sababu iliyomtoa kwenye reli. Kwa msimu huu wa 2020/21 hajafanikiwa kutupia ndani ya Ligi Kuu Bara.


Huenda mipango ya Namungo ikijibu ya kumuhitaji nyota huyo kwa mkopo anaweza kuendeleza makali yake kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Hemed Morroco.

SOMA NA HII  KIPA MWADUI ABEBESHWA ZIGO LA MABAO, AWEKA REKODI YA DAKIKA 900