Home Yanga SC OHOO..!! HUYO FISTON SASA MAMBO NI ‘BARIDIII’ HUKO YANGA

OHOO..!! HUYO FISTON SASA MAMBO NI ‘BARIDIII’ HUKO YANGA


Straika mpya wa Yanga, Fiston Abdulrazack aliyekosa mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliomalizika kwa sare ya 3-3, mambo yake freshi baada ya kupewa muda na benchi lake la ufundi kujiweka fiti ili arejee uwanjani akiwa kamili gado.

Fiston aliyesajiliwa dirisha dogo amecheza mechi moja tu dhidi ya Mbeya City na baada ya hapo hajaonekana tena uwanjani na kuzua sintofahamu kwa mashabiki, lakini mmoja wa viongozi wa Yanga wamelidokeza gazeti la  Mwanaspoti, mshambuliaji huyo Mrundi hakuwa fiti kwenye kiwango chake.

“Hajawa fiti, kocha alimpa muda ijiweke sawa, kwani hata alipocheza kwenye mechi mbili, ikiwamo ya kirafiki dhidi ya African Sports na ile ya Ligi, alikuwa akigongwa kidogo tu anapoteza muelekeo, kuonyesha anatakiwa kujifua zaidi. Ila kwa sasa kila kitu kipo freshi kwake na huenda akacheza mechi ya leo (jana) dhidi ya Mtibwa Sugar,” alisema kiongozi huyo ambaye anahusika pia na benchi la ufundi.

SOMA NA HII  YANGA YAENDELEA KUNG'ANG'ANIA UBINGWA WA LIGI KUU BARA