HABARI ZA SIMBA-KAGOMA
Habari za Simba Leo

YANGA YAMSAMEHE MCHEZAJI WA SIMBA

Abubakar September 6, 2024 4:22 pm

USAJILI wa kiungo Yusuph Kagoma ulikuwa na sintofahamu mwanzoni, kabla ya kutambulishwa rasmi na Simba kama mchezaji wao halali.

Awali kulikuwa na Taarifa za kwamba klabu ya Yanga, ilimsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa awali kabla ya Simba kuingilia dili la mchezaji huyo.

Mambo yapo hivi, Menejimenti ya mchezaji Yusuph Kagoma imeushukuru uongozi wa Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said kwa kumsamehe mteja wao ili aendelee kuitumikia Klabu ya Simba.

Yanga imeondoa shauri lake dhidi ya Kagoma katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ambapo mchezaji huyo alishitakiwa kwa kufanya udanganyifu baada ya kusaini pamoja na kupokea sehemu ya malipo kutoka klabu ya Yanga lakini akaenda kujiunga na Simba.

Taarifa iliyotolewa na menejimenti ya Kagoma, imethibitisha kumalizika kwa sakata hilo.

TP MAZEMBE YAMUOMBA STRAIKA WA YANGA WYDAD YARUDI TENA KWA MZIZE NA BIL 2.1