Home Habari za michezo OMBI LA KIBADENI KUTAKA ‘KUWATEMEA MATE ‘ MASTAA WAPYA SIMBA LAJIBIWA HIVI…

OMBI LA KIBADENI KUTAKA ‘KUWATEMEA MATE ‘ MASTAA WAPYA SIMBA LAJIBIWA HIVI…

Habari za Michezo

ALIYEKUWA Mshambuliaji na kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni ametaka kuonana na washambuliaji wa Simba ikiwemo wazawa ili kuzungumza nao na kuwapa baraka zake.

Amesema anatamani msimu wa 2024/25 kuona mshambuliaji mzawa ndani ya kikosi cha Simba kuweza kufikia na kuvuka rekodi yake ya kufunga hat trick katika mchezo wa watani dhidi ya Yanga.

Washambuliaji wazawa wanaongoza safu ya ushambuliaji ya Simba ni Valentino Mashaka, Kibe Denis, wakigeni wakiwa Leonel Ateba na Steven Mukwala.

Kibadeni amesema anaimani kubwa na Simba ya msimu huu kufanya vizuri na angependa kuonana na wachezaji wa timu hiyo kuwapa maneno kuhusu kuithamini nembo ya Simba.

Amesema lakini angependa kukutana na washambuliaji wa timu hiyo hasa wazawa ili kuwapa baraka zake na kufanikiwa kufunga mabao matatu katika mchezo dhidi ya Yanga.

“Nimeangalia mechi za Simba nimesikia kuna mshambuliaji mrefu kuliko goli anafunga tu Waahh!, sasa natamani washambuliaji hao ikiwemo wazawa kuletwa kwetu kwa ajili ya kuwapa maneno na baraka zangu.

Tangu nilipowafunga Yanga hat trick miaka ya nyuma hakuna aliyeweza kuweka rekodi hiyo, ningependa wazawa waje niwape baraka hizo ,” amesema Kibadeni.

Katika hatua nyingine Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amelipokea ombi hilo na kufanyia kazi kwa kuhakikisha vijana hao wanapata baraka hizo.

Mchezo wa watani wa jadi unayarajiwa kucheza Oktoba 19, 2024 Simba atakuwa nyumbani dhidi ya Yanga katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

SOMA NA HII  GAMONDI ATAMBA KUHUSU UBINGWA WA MSIMU HUU YANGA